Kama Chadema wana mikakati inayoisumbua CCM; inayoisumbua Serikali au inayovisumbua vyama vingine vya siasa, basi kuna mtu nyuma ya pazia anayebuni na kuratibu mipango hiyo.
Si mwenyekiti Freeman Mbowe, mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu wala kiongozi mwingine yeyote anayebuni mipango hiyo peke yake bila ya kumshirikisha ‘mchawi’ huyo.
Ni John Mrema; yule kada aliyekuwa anaendesha mikutano yote ya kampeni za urais za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ndiye mchawi wa mikakati ya Chadema kwa sasa ndani na nje ya Bunge.
Mrema ni kada wa Chadema ambaye alikuwa meneja wa kampeni za urais za Lowassa, ambayo iliundwa na CUF, NCCR-Mageuzi, NLD na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Ndani ya Chadema, Mrema sasa ni mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje na kabla ya kupewa cheo hicho, alikuwa mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri.
“Mimi si mchawi, lakini habari za Chadema hazikauki kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari. Nataka muende wenyewe mkafanye utafiti muone jinsi Chadema inavyotawala kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mrema .
Sign up here with your email