Meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema wamachinga waendelee kufanya biashara mjini na wasibughudhiwe na mtu yoyote.
Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri
wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.
Hivi
karibuni alipokuwa Mwanza, Rais John Magufuli aliruhusu wafanyabiashara
hao waendelee kufanya kazi kati kati ya mji hivyo hata wa jijini hapa
wanaguswa na kauli hiyo.
Sign up here with your email