Wananchi wanaoishi katika Kata ya Nyasaka a,b,na c, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa kivukio yaani daraja katika Mto Nyakurunduma ambao unatiririsha maji katika Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Wananchi hao Wamesema tatizo hilo limekua kero kubwa ya miaka mingi kwani mvua zikinyesha mto huo hufurika kiasi cha kusababisha wananchi kushindwa kuvuka mto huo mara kwa mara na wakati mwingine kwa Wanafunzi kupitwa na masomo, imeelezwa kuwa hivi karibuni wanafunzi watatu na madereva wawili wa pikipiki walisombwa na maji wakati wakivuka katika mto huo na kupoteza maisha.
aidha wananchi hao wamesema walipofikisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, aliwahakikishia tatizo hilo lingefanyiwa kazi baada ya mvua kupungua lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika badala yake wananchi hao wamelazimika kujenga daraja la miti ili wapate sehemu ya kuvukia kwani muda wowote mvua zinaweza kuanza tena.
Muonekano wa Daraja hilo lililojengwa na Mwananchi wa Kata ya Nyasaka a,b,na c, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Watoto wakivuka.
MO DEWJI AMWAGA MILIONI 100 ZA USAJILI SIMBA SC JIJINI DAR LEO
Mfanyabiashara
maarufu nchini, Mohammed Dewji ameanza kuinufaisha klabu ya Simba
baada ya kuipatia sh milioni 100 kwa ajili ya kusaidia zoezi la
usajili.
Dewji alikabidhi fedha hizo kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited zilizopo jengo la Golden Jubilee,jijini Dar. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Dewji alisema kuwa fedha hizo ni mchango wake kwa timu hiyo ili kusajili wachezaji ambao imepanga kuwaongeza katika zoezi ambalo litaisha Agosti 6.
Dewji alisema kuwa amefurahishwa sana na hatua ya uongozi na wanachama wa klabu hiyo kubariki mabadiliko ya uendeshaji na kuingia katika mfumo wa hisa. “Huu ni mchango wangu kama mwanachama wa klabu, nina mambo mengi mazuri yanakuja wakati wa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu,” alisema Dewji.
“Simba SC ni timu kubwa sana, ina wanachama na mashabiki wengi, inahitaji kuwa na hadhi ya pekee kabisa, naamini kwa mchango huu, uongozi utaweza kumsajili mchezaji kutoka Ivory Coast ambaye kwa sasa anasubiri fedha ili aweze kusaini,” alisema.
Rais wa Simba, Evans Aveva alimshukuru Dewji kwa msaada huo ambao utawawezesha kumsajili mchezaji, Frederick Blagnon. Alisema kuwa kwa sasa klabu yao inahitaji Sh milioni 320 ili kukamilisha usajili na kuwaomba wadau wengine kumuunga mkono Dewji.
Mfanyabiashara
maarufu nchini Mohamed Dewji akimkabidhi mfano wa hundi sh. milioni 100
Rais wa Simba SC, Evans Aveva kama mchango wake katika usajili wa klabu
hiyo leo ofisini kwake,jijini Dar es salaam.PICHA NA MICHUZI JR.
Mfanyabiashara
maarufu nchini Mohamed Dewji a.k.a Mo Dewji akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akikabidhi mfano wa
hundi ya sh. milioni 100 kwa Rais wa simba sc,(pichani kushoto) Evans
Aveva kama mchango wake katika usajili wa klabu hiyo.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
Sign up here with your email