BURUNDI IMEPINGA KUTUMWA KWA POLISI WA UN KULINDA AMANI - Rhevan Media

BURUNDI IMEPINGA KUTUMWA KWA POLISI WA UN KULINDA AMANI

Serikali ya Burundi imepinga kutumwa kwa kikosi cha polisi wa umoja wa mataifa katika taifa hilo, katika juhudi za kumaliza machafuko ya kisiasa yaliodumu kwa mwaka mmoja sasa. Burundi imepinga kutumwa kwa polisi wa kulinda usalama wa UN
Serikali ya Burundi imepinga kutumwa kwa kikosi cha polisi wa umoja wa mataifa katika taifa hilo, katika juhudi za kumaliza machafuko ya kisiasa yaliodumu kwa mwaka mmoja sasa.
Juma lililopita , baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipitisha mswada uliopendekezwa na Ufaransa, wa kutuma maafisa 228 wa kulinda amani katika taifa hilo ndogo la kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Burundi inasema imekataa azimio hilo, ikisema linakiuka uhuru wake.
Serikali ya Burundi inasema vyombo vyake vya usalama vinadhibiti hali inavyohitajika.
Burundi inashikilia kuwa hali ilivyo haitaji askari zaidi ila inaweza tu kuwaruhusu wachunguzi wasiozidi hamsini kuingia nchini humo.
Zaidi ya watu 400 wameuawa tangu rais Pierre Nkurunziza aamue kuwania urais kwa muhula wa tatu Aprili mwaka wa 2015.
Zaidi ya watu 200,000 wametorokea mataifa jirani kufuatia ghasia zilizofuatia tangazo la rais Nkurunziza.
Wafuasi wa serikali na wale wa upinzani pia wameuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi baina ya wafuasi hao.
Previous
Next Post »