June 30 2016 Mbunge
wa Singida Mashariki, ‘CHADEMA’ Tundu Lissu amesomewa shitaka lake la
kutoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu June 28
2016 kinyume cha kifungu namba 32 ya sheria ya magazeti. Lissu amekana
shtaka hilo na ameachiwa kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.
Inadaiwa
Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu kwa kumuita
Rais ‘dikteta uchwara’, mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili na
kesi imeahirishwa mpaka August 02 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa. Nje
ya mahakama ya Kisutu, Lissu ameyazungumza haya……….
>>>>’mimi
nilidhani kwamba baada ya kauli yangu wenye busara wangenyamaza kimya
lakini inaelekea busara inaonekana ni bidhaa adimu wameyaleta
mahakamani, mimi na jopo langu la mawakili tutapata fursa ya kumuita
huyo niliyemuita dikteta ‘uchwara’ kuja mahakamani kuiambia mahakama
kuwa yeye si dikteta uchwara‘
Sign up here with your email
