Mwanasiasa mmoja
kutoka katika chama tawala nchini Bangladesh ameeleza masikitiko na
hisia za aibu baada ya kugundua kuwa mtoto wake wa kiume ni miongoni mwa
kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la Islamic State walioshambulia
mgahawa mmoja katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka, mwishoni mwa juma
lililopita, na kuua watu ishirini na wawili.
Imtiaz Khan ameiambia
BBC kwamba mwanawe huyo wa kiume, aitwaye Rohan, aliondoka nyumbani
kwake miezi sita iliyopita.Zaidi ya hayo amewapongeza polisi na serikali
ya nchi hiyo kwa kuendesha uchunguzi na hatimaye kumtia mkononi kijana
huyo, na amesikitika kusikia kwamba mmoja wa askari polisi aliyekuwa
katika harakati za kumkamata kijana huyo alijeruhiwa.Rohan na wenzake ambao wamefariki dunia wanatoka katika familia maarufu nchini humo na wengine wamesomeshwa ughaibuni.
Kundi la Islamic State lilitupia picha ya Rohan kuwa ndiye aliyetekeleza shambulio hilo, wakati walipokuwa wanatoa tamko la kuhusika na tukio hilo.
Sign up here with your email