Morocco imetoa tamko la nia yake ya kutaka kujiunga tena katika umoja wa Afrika.
Katika
ujumbe uliotumwa kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Matataifa ,mjini
Kigali, Rwanda, Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita amesema sasa ni
wakati muafaka kwa taifa lake kurejea na kuchukua nafasi yake katika
jumuiya hiyo ya umoja wa Afrika.Morocco ilijitoa katika umoja huo mwaka 1984 wakati umoja huo ulipotambua uhuru wa eneo la magharibi mwa sahara.
Morocco ilidai kuwa eneo la Magharibi mwa Sahara lilikuwa ndani ya mipaka yake.
Hata hivyo Umoja wa Afrika umesema utaendelea kusukuma upatikanaji wa haki ya watu wa eneo la Magharibi mwa Sahara ili kuwa na uhuru kamili bila kuingiliwa
Sign up here with your email