Wanachama wa Klabu ya Yanga
ghafla waliugeuza zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo uliofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kama harambee ya baada ya kuamua
kuchanga fedha kwa ajili ya ujezi wa uwanja.
Ilikuwa ni baada ya msemaji wa klabu
hiyo, Jerry Muro aliyekuwa akiongoza shughuli nzima kwenye uchaguzi
kusema kuwa serikali ya awamu ya nne imewanyanyasa kwa kuwanyima kibali
cha kuanza ujezi wa uwanja mbele ya DC wa Ilala, Raymond Mushi ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi hilo.
Kusema hivyo, wanachama walilipuka kwa
kelele, kisha kuanza kumpelekea Murro stejini na kumuagiza amkabidhi DC
ambaye pia alikuwa ameketi na Wajumbe Wakuu wa Bodi ya Udhamini, Mama
Karume na Francis Kifukwe.
Haikujulikana mara moja kuwa ni kiasi
gani cha fedha kilichochangwa leo kwa ajili ya kutimiza adhima hiyo ya
kujenga uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ya Yanga.
Sign up here with your email
