Wapenzi wa jinsia
moja nchini Ivory Coast wamekuwa wakidhulumiwa na kulazimishwa kuhama
makwao baada ya ubalozi wa Marekani kuchapisha picha yao wakiweka sahihi
kwenye kitabu cha rambi rambi kwa waathiriwa wa mauaji yaliyofanyika
katika klabu moja ya wapenzi wa jinsia moja mjini Orlando jimbo la
Florida nchini Marekani.
Picha iliyochapishwa kwenye mtandao wa
ubalozi wa Marekani na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ilionyesha
wanaume sita wakiweka sahihi kwenye kitabu cha rambi rambi.Shirika la habari la AP lilizungumza na wanaume hao wote wanne ambao hawakutaka kutajwq majina.
Wawili kati yao wanasema kuwa walisambuliwa na kundi la watu huku wengine wawili nao wakisema kuwa shinikizo za kifamilia zimewalazimu kuhama nyumbani.
Sign up here with your email
