Meneja utetezi kutoka Shirika
la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu
ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri
sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi.
Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia
wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya
tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa wanawasikiliza wenzao wakati walipokuwa wanawasilisha mada walizopewa
Muwezeshaji kutoka Forum CC
Feizal Ally Akiongoza majadiliano juu ya uandaaji wa bajeti ya kilomo na
mabadiliko ya tabianchi ambayo yanawathiri kwa kiasi kikubwa wakulima
wadogo wadogo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa
Baadhi ya washiriki wa semina
hiyo ambao ni wakulima wadogo wadogo wakichangia mada juu ya changamoto
wanazozipata katika kuandaa Bajeti na kutoshirikishwa
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakichangia juu ya mabadiliko ya Tabianchi yanavyosababisha athali katika kilimo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Picha na Fredy Njeje
Dar es salaam, Wanawake
wakulima wadogowadogo wakiongozwa na waliokuwa washiriki wa Shindano la
Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na shirika la Oxfam, wamekutana
pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na baadhi ya wanafunzi kutoka
elimu ya juu, Tanzania kujadili Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17 na
changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Akifungua Mkutano huo wa siku tatu,
Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka Kibona alisema kuwa lengo
la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya majadiliano juu ya
Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali ilivyo sasa
ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya
kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia
kuibua changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau
suala la mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa
katika kilimo.
Akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema mabadiliko ya
Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo wadogo
hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu
ili kukabiliana na mabadiliko hayo.
Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko
ya tabia nchi mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba
changamoto kubwa zaidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji
chumvi kuingia nchi kavu na kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa
joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua kwa kina cha maji katika
mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja
na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao.
Alisema kuwa mambo yote hayo yamekuwa
yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya malisho kwa ajili ya
mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana na changamoto
hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali
ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi ya
mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto,
matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.
Nao wakulima hao kwa nyakati
tofautitofauti walizungumzia suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa
changamoto nyingi wanazozipata kwa kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu
ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na elimu na huduma mbalimbali
zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo basi kupitia
mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji wa
bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya
kilimo nchini.
Sign up here with your email
