WACHEZAJI 8 WALIOBADILI URAIA NA KUCHEZEA MATAIFA MENGINE. - Rhevan Media

WACHEZAJI 8 WALIOBADILI URAIA NA KUCHEZEA MATAIFA MENGINE.

Diego Costa
8.Thiago Motta (Brazil kwenda Italy).
Thiago Motta ni Mbrazil wa pili kubadili na kuchukua uraia wa taifa lingine, baada ya kuichezea Brazil kwenye michuano ya CONCACAF Gold Cup mwaka 2003.
Thiago (33) alizaliwa kunako eneo la Sao Bernardo do Campo, nchini Brazil. Aliichezea timu ya taifa ya Brazil chini ya miaka 23, lakini hakupata nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi cha wakubwa.
Babu mzaa babu yake alikuwa ni raia wa Italy. Mchezo wake wa kwanza kwa taifa la Italy ulikuwa ni mwaka 2011, aliiwakilisha Italy kwenye michuano ya Euro mwaka 2012 na Kombe la Dunia mwaka 2014. Bado ni sehemu ya kikosi cha Italy kinachoshiriki Michuano ya Euro mwaka huu inayofanyika nchini Ufaransa.
  1. Pepe (Brazil kwenda Ureno)
Pepe alizaliwa nchini Brazil lakini alihamia nchini Ureno akiwa na umri wa miaka 18 kujiunga na klabu ya C.S Maritimo.
Kamwe hajawahi kuitwa katika timu ya taifa ya Brazil mpaka alipoamua kubadili uraia wake, lakini kwa mujibu wa ripoti mbalimbali wakati fulani Pepe alifuatwa na Dunga ili aweze kumwita katika kikosi chake lakini alikataa kwa kuwa tayari alikuwa ameshafanya maamuzi ambayo anahisi yalikuwa sahihi.
6. Jonathan De Guzman (Canada kwenda Uholanzi)
De Guzman alizaliwa nchini Canada huku baba yake akiwa na asili ya Ufilipino na mama yake Mjamaica.
Mchezaji huyo wa zamani wa Vallarreal alipata makuzi yake nchini Canada mapaka alipofikisha umri wa miaka 12, baadaye alihamia nchini Uholanzi kujiunga na timu ya vijana ya Feyernood.
Alikuwa na uhalali wote wa kuchezea Canada, Ufilipino na na Jamaica lakini alichagua kuchezea Uholanzi. Alifanikiwa kupata uraia mwaka 2008.
  1. Neven Subotic (USA kwenda Serbia)
Beki huyu wa Dortmud aliazaliwa Yougoslavia, na wazazi wenye asili ya Bosnia, alikuwa na uhalali wa kuwakilisha taifa la Bosnia Herzegovina au Serbia.
Wakati wa vita vya Serbia, familia yake ilihamia Ujerumani  halafu baadaye kwenda nchini Marekani na kupata uraia wa nchi hiyo.
Akiwa kijana mdogo, Subotic alicheza klabu za Sparta Gold na Impact Black. Hata hivyo aliamua kuchagua kuchezea Serbia.
  1. Miroslav Klose (Poland kwenda Ujerumani)
Huyu ni mfungaji bora wa muda wa muda wa Michuano ya Kombe la Dunia. Alizaliwa Poland lakini familia yake ilihamia nchini Ujerumani wakati akiwa na umri wa miaka 8. Alikuwa na uhuru wa kuchagua taifa lolote kati ya haya mawili lakini kalamu yake ilidondokea kwa Ujerumani.
  1. Kevin-Prince Boateng (Ujerumani kwenda Ghana)
Kevin-Prince Boateng ni kaka wa mchezaji wa Ujerumani Jerome Boateng. Baba yake alikuwa ni raia wa Ghana wakati mama yake alikuwa ni Mjerumani. Alipata makuzi yake nchini Ujerumani na kuanza maisha yake ya soka katika klabu ya Hertha BSC.
Amewahi kucheza timu za taifa za Ujerumani chini ya Umri wa miaka 19 na 21. Lakini ilipofika wakati wa kufanya maamuzi ya kuchezea timu ya wakubwa, aliamua kuchagua Ghana.
  1. Lukas Podolski (Poland kwenda Germany)
Lucas Podolski, ambaye kwa sasa anacheza kunako klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, alizaliwa nchini Poland; na wazazi wake walihama naye kwenda Ujerumani wakati akiwa na umri wa miaka 2, na baadaye alianza kucheza mpira akiwa na timu ya FC Koln mwaka 2003.
Kuna wakati aliomba kuchezea timu ya Poland lakini kocha wa Poland kwa wakati huo Pawel Janas alitilia shaka uwezo wake na kumpuuza. Podolski baadaye aliamua kuchezea Ujerumani.
  1. Diego Costa (Brazil kwenda Uhispania)
Straika wa Chelsea Diego Costa ni moja ya wachezaji wanaochukiwa mno kwa sasa ulimwenguni kutokana na utukutu wake uwanjani, lakini vile vile kwa kupiga chini uraia wa timu yake.
Costa (27) aliiwakilisha Brazil kwenye michezo miwili tu ya kirafiki mwaka 2013, lakini aliomba uraia wa Uhispania baadaye mwaka uliofuata akapata fursa ya kuiwakilisha timu ta taifa ya Uhispania kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Previous
Next Post »