|
VIONGOZI wa vijiji akiwemo Mtendaji wa kata ya Migato
wilaya Itilima Mkoani Simiyu, wametuhumiana kutafuna zaidi ya shilingi Milioni
saba zilizokuwa za ujenzi wa maabara mbili zilizomo kwenye kata hiyo.
Viongozi hao
walitumia muda wa saa sita kurushiana mpira kwa kila mmoja kuhusika na
ubadhilifu wa fedha hizo, hali iliyosababisha kuanza kutaja siku, wakati na
mahali walivyotafuna fedha hizo.
Hali hiyo
ilijitokeza juzi wakati wa kikao cha maendeleo cha kata (WODC) kilichokuwa
chini ya Diwani wa kata hiyo Mbuga Ntobi, pamoja na Kaimu mkurugenzi wa
halmashauri Anneth Msofe.
Awali
akizungumzia hali ya maabaara hizo katika shule ya sekondari Shishani, pamoja
na Mhunze, Diwani huyo alieleza kuwa tangu ameingia madarakani hakuna
mwendelezo wa ujenzi wa maabara hizo.
Alieleza kuwa
alishangazwa kuona mbao kwa ajili ya kuezeka mabaara zote mbili zikiwa tayari
zimeungwa, huku ujenzi wa boma ukiwa katika kozi mbili na kasi yake ikiwa
katika kiwango cha chini.
“ Mpaka leo mbao
ziko chini zimeungwa na leo ni muda wa mwaka mmoja umepita mbao hizo zimeanza
kuoza huku ujenzi ukiwa katika kozi mbili za boma nimekuwa nauliza kwa nini
ujenzi umesimama? sijapata jibu sasa leo
lazima tupate jibu hapa hapa” alisema diwani
huyo.
Baada ya diwani
kutoa maelezo hayo alimtaka Mtendaji wa kata Logo Sitta kutoa majibu, ambapo
alianza kusoma fedha zilizopatikana na matumizi yake wakati wa ujenzi wa
maabara hizo.
Taarifa hiyo
ilikataliwa na wajumbe wa kikao hicho ambao baadhi yao walikuwa wenyeviti wa
vijiji, ambapo walianza kusoma taarifa za kwao ambazo zilikuwa zinakinzana na
taarifa ya mtendaji wa kata.
Ndimila Buhula
pamoja na Linja Tulutu walieleza kuwa Mtendaji huyo wa kata ndiye chanzo cha
ujenzi wa maabara hizo kushindwa kuendelea kutokana na kushindwa kutoa matumizi
sahihi ya fedha zilizotoka halmashauri kwa ajili ya ujenzi.
Hatua hiyo
ilimfanya Mtendaji wa kata kuanza kueleza jinsi fedha hizo zilivyotumika,
ambapo alibainisha kuwa baadhi ya fedha walitumia kwa ajili ya kupeana posho
usafiri pamoja na chakula kwenye vikao vya wajumbe wa kamati ya ujenzi wa
maabara .
.
Hali hiyo ilizua
mzozo mkubwa kutoka kwa wenyeviti hao ambao walikana na kudai kuwa vikao vyote
kwenye kamati hawajawahi kula chakula wala kupewa posho, huku wakieleza
walimsikia mtendaji akiomba ten Parcent (rushwa) kutoka kwa mkandarasi alipewa
kazi ya ujenzi.
Mbali na hilo
walieleza kuwa mtendaji huyo alisaidia Mkandarsi huyo kukimbia na fedha za
ujenzi ambazo alilipwa na mtendaji bila ya kuwepo wajumbe, na mpaka leo
mkandarasi wahajui mahali alipo.
Baada ya hali
hiyo ilibainika kuwa jumla ya shilingi Milioni 7,430,250 zilitafunwa na
viongozi hao wakiongozwa na mtendaji wa kata, ambapo kikao kiliazimia warejeshe
fedha hizo mara moja.
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye pia ofisa utumishi,
alimtaka mtendaji wa kata kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa haraka na hatua za kisheria zitachuliwa dhidi yake.
|