DAR ES SALAAM: Uchumba wa staa
wa wimbo wa Chura, Snura Mushi na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Ally
umevunjika kabla hata wazazi wa msanii huyo hawajatoa majibu ya barua ya
posa.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuvunjika
huko kunatokana na muoaji huyo kumweleza wazi Snura kuwa, katika maisha
yao ya ndoa, yeye hatahusika na matunzo ya watoto wawili ambao staa huyo
wa muziki amezaa na wanaume wengine.
“Ndiyo kwanza huyo Ally alikuwa
amepeleka posa nyumbani kwa wazazi wake Snura, Mwananyamala (Dar) na
ilishapokelewa, alikuwa akisubiri jibu ili kama wakikubali aoe, lakini
kwenye uchumba wao ndiyo akamwambia mwenzake hivyo, naye akaona hawezi
kukaa na mwanaume ambaye hawataki watoto wake,” kilidai chanzo hicho.
“Kumbe hamjainyaka hii habari? Iko hivi
kuna jamaa anaitwa Ally ndiye alimchumbia Snura. Alimtuma mshenga wake
anaitwa HK (meneja wa Snura) kwenda kumuwakilisha katika suala zima la
kutoa posa,” kilidai chanzo hicho huku kikiomba hifadhi ya jina.
Chanzo hicho kikasema: “Lakini sasa
uchumba umevunjika na hakuna ishu tena. Hii ni kama mkosi kwa Snura
japokuwa hata mwenyewe Snura alikuwa radhi kwa sababu alizosema jamaa.”
Baada ya kunasa ubuyu huo, Risasi
Jumamosi lilimvutia waya HK ambapo alipopatikana alikiri kwenda kutoa
posa na kuongeza kwamba, uchumba huo ulivunjika muda mfupi baada ya
jamaa kuweka wazi kwamba, anamtaka Snura tu na si watoto wake.
Mama Snura
“Si unajua misimamo, jamaa alitaka kuwa
na Snura na si watoto, Snura akaona hawezi kuwatupa watoto wake, anataka
kuwalea mwenyewe, na yeye akasema uchumba ufe tu,” alisema HK.
Alipoulizwa Snura kuhusu tukio hilo,
alisema alipokea kwa mikono miwili uchumba huo lakini alishangaa msimamo
wa mtarajiwa wake huyo wa kutotaka watoto.
“Kuolewa ni jambo la kheri lakini
watoto pia ni baraka. Sasa kama mwenzako hataki watoto wako nini
kitaendelea? Hata mimi sikuwa radhi, uchumba ukafa,” alisema Snura.
Kabla ya kuchumbiwa na Ally, Snura
alishazaa na wanaume wawili tofauti ambao wote safari yao iliishia
njiani baada ya kumwagana kwa kushindwana tabia.
Sign up here with your email
