Iwapo kura hiyo itapitishwa, serikali ya Uswisi itakuwa ikiwalipa raia wake ambao wanaishi nchini humo kihalali, kiasi cha dola 2,500 kila mwezi sawa na shilingi 5,476,750 za kitanzania , hata ikiwa wameajiriwa au la.
Baadhi ya wachanganuzi wa kiuchumi wanasema kuwa mfumo huo, utawasaidia
pakubwa na bado utaiwezesha serikali kusalia na fedha katika hazina yake
ya taifa.
Wanauunga mkono wanasema kwamba, hatua hiyo itasaidia pakubwa
kukabiliana na umaskini na kuwapa watu uwezo wa kuamua namna wanavyoishi
na kufanya kazi.
Lakini wanaoupinga miongoni mwao vyama vyote vikuu nchini Uswizi,
wanahoji kuwa fedha hizo zitawafanya watu kuzembea bila ya kufanya kazi.
Sign up here with your email
