UONGOZI WA KLABU YA YANGA WAKUBALI MATOKEO, KUINGIA MSITUNI JULAI MOSI, WAPANIA KUFANYA VIZURI . - Rhevan Media

UONGOZI WA KLABU YA YANGA WAKUBALI MATOKEO, KUINGIA MSITUNI JULAI MOSI, WAPANIA KUFANYA VIZURI .

BAADA YA kupoteza michezo miwili sasa kikosi cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Julai mosi kwa ajili ya maandalizi yao ya mechi zake za kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo kambi hiyo itakuwa nje ya Jiji la Dar es salaam huku wakiwa hawajaweka bayana ni wapi wataelekea. 
 Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry muro amesema kuwa wachezaji wamepewa siku mbili za mapumziko na Julai mosi kikosi kitaingia kambini. na tayari benchi la ufundi limeshakutana na uongozi na kuzungumzia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo na baada ya kuona makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao uliopita dhidi ya TP Mazembe sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo wao huo ili kuhakikisha wanafanya vizuri. 
 Kwa sasa timu yao imebakiza mechi nne katika hatua hiyo hivyo maandalizi yatakayofanywa ni makubwa na watahakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao uliosalia dhidi ya Medeama pamoja na mechi za marudiano. 
"Kikosi kitaingia kambini kujiandaa na michezo yetu na tutahakikisha maandalizi yanayofanyika yanakuwa ya hali ya juu ili kuweza kupata pointi tatu katika kila mchezo", amesema Muro.
 Mechi inyofuata ya Yanga ni dhidi ya Medeama ya Ghana huku pia ikisubiri michezo yake ya marudiano na kufanya idadi ya michezo hiyo minne. 
 Licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao kwa nguvu zote lakini walishindwa kutumia nafasi walizozipata katika dakika 45 za kwanza na matokeo waliyoyapata ndo yameshatokea na hawawezi kubasilisha ukweli kuwa wamepoteza mchezo huo muhimu kwao tena katika uwanja wa nyumbani na zaidi uongozi wameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wao hivyo hawana sababu ya kumlaumu mtu kwa kupoteza mchezo huo. 
 Katika hatua nyingine Jerry alisema kuwa anataka wanayanga watambue kuwa madai ya wao kutakiwa kulipa deni la zaidi ya milioni 530 hazina ukweli wowote kama mchezo huo ulikuwa bure na hawakuingiza mapato yoyote, watatakiwaje kulipa deni hilo, 
"Kinachotuhusu sisi ni kulipia gharama za uwanja pamoja na vivu vingine muhimu hivyo kama kuna uharibifu wowote basi asilimia 15 ya fedha tunazolipa yatatumika kwa ajili ya uharibifu huo".




Previous
Next Post »