Balozi Mdogo wa India Zanzibar Balozi T
C.Barupal, akisalimiana na Mgeni rasmin wa Maadhimisho ya Siku ya YOGA
yaliofanyika Zanzibar, Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe
Rashid Ali Juma akiwasili katika ukumbi wa ZanCinema Malindi Zanzibar,
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma akisalimiana na Maofisa wa Ubalozi wa India Zanzibar
Balozi Mdogo wa India Zanzibar
akisalimiana na Balozi Mdogo wa Msumbuji Zanzibar wakati wa hafla hiyo
ya Siku ya YOGA iliofanyika katika ukumbi wa ZanCinema Malindi Zanzibar.
ZGFCCM Yatowa Elimu ya Maradhi ya HIV, TB na Maralia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utalii
Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Chuom Kombo akifungua Semina ya siku
moja ilioandaliwa na ZGFCCM kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
kuhusiana na Maradhi ya HIV, TB na Malaria, iliofanyika katika ukumbi
mdogo wa Baraza chukwani Zanzibar kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na kulia Makamu Mwenyekiti wa ZGFCCM
fedha Ndg Hassan Ali Mzee.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na
Michezo akifungua Semina hiyo ya Siku moja.
Makamu Mwenyekiti wa ZGFCCM,Bi
Benedicta Maganga
akitowa
muhtasari wa Global Fund na ZGFCCM wakati wa semina hiyo kwa wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi mdogo wa
Baraza Chukwani Zanzibar.
Wajumbe wakifuatilia maelezo wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibarwakifuatilia Mada inayowakilishwa
katika Semina hiyo ya Siku Moja kuhusiana na Maradhi ya HIV, TB na Malaria,ilioandaliwa na Taasisi ya ZGFCCM.
Mkurugenzi wa Huduma za Hospital Zanzibar Dk Mohammed Dahoma, akitowa mada kuhusiana na
Maambukizo ya HIV, TB na Malaria, wakiti wa semina
hiyo ilioandaliwana Taasisi ya ZGFCCM kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kutowa elimu ya maradhi hayo iliofanyika
katika ukumbi mdogo wa Baraza Chukwani Zanzibar
KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na
Usajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akiuliza swali wakati wa
kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano
kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo
Mkubwa na Wanawe watoa msaada Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke
Kituo
cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe,
kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa mbalimbali vikiwe vile vya
usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya Watoto waliolazwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Awali
akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho,
Said Fella, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na
changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke ambayo pia ni majirani
zao ambapo pia amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa likifika
Hospitalini hapo kuchangia misaada mbalimbali.
Said Fella ameongeza kuwa, alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.
“Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema Fella.
Serikali Haitamuonea Muhali Yoyote Atakayehusika na Uingizaji wa Dawa za Kelevya Nchini.
Na. Miza Kona Maelezo – Zanzibar.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari
zitazokamatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya kwa lengo la
kudhibiti uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa hizo nchini .
Akizungumza
kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Waziri Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed huko Mnara wa
kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na
Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali
haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa
za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza
nguvu ya Taifa.
Amesema
wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni
wahujumu wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto
na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu
bila ya kuwaonea muhali.
Ameeleza
kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi
yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa
ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na
kupoteza viungo muhimu vya mwili.
Sign up here with your email