NYOTA
wa Bongo Fleva na Bosi wa lebo ya Poz kwa Poz ‘PKP’, Omary Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’, amesema moja ya matukio ambayo hawezi kuyasahau ni siku
aliposwekwa lupango huko Marekani kwa kosa la kutumia vibaya hati yake
ya kusafiria.
Akibonga
na Swaggaz hivi karibuni, Ommy Dimpoz, alisema alikuwa anatokea
Uingereza kwenda Marekani, viza aliyokatiwa na promota wake ilikuwa ni
ya kwenda kutalii na siyo kufanya kazi kama mwenyeji wake huyo alivyo
mdanganya.
“Nilipofika
uwanja wa ndege nilishangaa kuambiwa nisubiri kwenye chumba tofauti na
wenzangu. Nikaanza kuhojiwa nitoe sababu za kuingia Marekani, mimi
nikasema nimekwenda kutembea.
Wakaomba
mawasiliano ya mwenyeji wangu, nikawapa ya promota, sijui waliongea
naye nini ila yule ofisa wa uwanja wa ndege aliporudi kwenye chumba kile
alikuja na askari polisi wawili na akaniambia nimedanganya nakwenda
kutembea wakati nakwenda kufanya kazi kitu ambacho ni kosa, kwa hiyo
nikawekwa chini ya ulinzi,” alisema Dimpoz.
Ommy
Dimpoz, anasema baada ya kutiwa nguvuni, akavishwa mavazi ya jela,
akapigwa pingu na kupelekwa jela ambako aliyafurahia maisha ya kule
kutokana vyakula vitamu wanavyopewa wafunga na baada ya hapo alirudishwa
Tanzania.
Sign up here with your email