Serikali imewataka maafisa
mipango miji watumie vyanzo vya ndani vya halmshauri pamoja na kutumia
taaluma kufanya mipango rafiki ya kijamii ili wananchi waishi katika
mipango bora na kuepuka majanga yanayoweza kuepukika.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jaffo.
Akizungumza
leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Naibu
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jaffo, amewataka wahikikishe maeneo
yao yote yanakuwa maeneo rafiki yaliypangwa vizuri kupitia taaluma zao.
Waziri Jaffo amekiri kuwa miji mingi inavyokuwa kunakuwa na ujenzi holela usiozingatia viwango na kuwataka maafisa hao kuacha kufanya kazi kwa kushinda maofisini na kutembelea maeneo ambayo yapo maalumu kwa ajili ya ujenzi uliobora.
Waziri Jaffo alikuwa anajibu swali la mbunge wa Nkasi Kusini Mhe. Deosderius Mipata aliyetaka kujua serikali imejipangaje katika kuudhibiti ujenzi holela unaoendelea katika miji tofauti nchini bila kuzingatia utaratibu.

Sign up here with your email