Kuna uwezekano mkubwa wa Scotland kupiga kura upya ya kujitenga na Uingereza.
Kiongozi
mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema kwamba kufuatia kura ya
kujiondoa kwa muungano wa EU, sasa ni bayana kuwa hatma ya baadaye ya
watu wa nchi yake wanajiona kuwa sehemu ya EU.Matamshi ya Sturgeon yanafuatia matokeo yaliyodhihirisha kuwa kila eneo wakilishi la Scotland lilipiga kura kusalia kwenye muungano wa Ulaya EU wala sio kujiondoa.
Mwenyekiti wa chama cha Irish Republican, Sinn Fein, maarufu kama (Declan Kearney), amesema kwamba kura ya Uingereza imechochea kesi ya kuitisha kura ya maoni kuhusiana na umoja wa Ireland.
Hata kabla matokeo hajakuwa bayana, wafuasi wa chama cha Conservative wa mrengo uliotaka Uingereza iondoke, wamertia saini taarifa ya gazeti moja inayomtaka waziri mkuu David Cameron kusalia ili kurekebisha kura hiyo ya maoni.
Naye kiongozi mkuu wa chama chama UK Independence, Nigel Farage, amemuomba Bwana Cameron kujiuzulu.
Sign up here with your email
