Rais wa Bunge la
Senate nchini Nigeria na naibu wake wamefikishwa mbele ya mahakama kwa
makosa ya kugushi, ambayo ina adhabu kali hasa kwa kuwa wao ni wanasiasa
watajika nchini humo.
Bukola Saraki na naibu wake Ike Ekweremadu,
wamekanusha madai hayo yanayoaminika kutekelezwa mwaka jana, ambayo
iliwasaidia kupata vyeo walivyo navyo sasa.Iwapo watapatikana na hatia, watahukumiwa kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Bwana Saraki pia, amekuwa akikabiliwa na kesi nyingine mahakamani kuhusiana na udanganyifu wa mali anayodaiwa kumiliki, makosa ambayo ameyakanusha.
Sign up here with your email