MANENO SELANYIKA NA BARAKA MASSAWE (TSJ), DAR
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) wa kambi ya
Lugalo, Hamis Omary (31), amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Kinondoni
akituhumiwa kumbaka mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka
minne.
Mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, wakili wa Serikali, Amani Mghamba, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei, 31 mwaka huu eneo la Kawe, Wilaya ya Kinondoni.
Akisoma hati ya mashtaka, wakili Mghamba alidai kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kilichomsababishia maumivu makali mtoto huyo.
Mtuhumiwa alikana shtaka linalomkabili na Hakimu Kiliwa alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo lina dhamana hivyo alimtaka mtuhumiwa awe na wadhamini wawili wanaotoka serikalini au katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
“Kila mdhamini anatakiwa aje na barua kutoka kwa mwajiri wake kisha wataweka ahadi ya maandishi ya Sh milioni 2 kwa kila mmoja,” alisema Hakimu Kiliwa.
Mtuhumiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na alirejeshwa mahabusu hadi Julai 8 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.

Sign up here with your email