Aliyekuwa
Mbunge Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amelalamikia kuhujumiwa baada ya
ofisi zake kwa nyakati tofauti kisha kumwibia nyaraka mbalimbali na mali
za thamani kubwa.
Matukio hayo yamefanyika kwa nyakati tofauti ambapo Machi
5, mwaka watu wasiojulikana walivunja ofisi yake iliyoko Posta katikati
ya Jiji la Dar es Salaam waliina vitu mbalimbali wakati tukio kama hilo
lilirudiwa Machi 13 katika ofisi yake ya Chang'ombe ambapo
zilichukuliwa nyaraka za uchaguzi wa mwaka jana pekee licha ya kuwa
kulikuwa na vitu vingine vya thamani kubwa.
Hali
kadhalika usiku wa kuamkia Juni, 26 (leo) wezi hao wameingia tena
katika ofisi hiyo baada ya kufanikiwa kumpa mlinzi chakula kinachodaiwa
kuwekwa dawa za kulevya ambapo alilala ndipo walipata mwanya wa kuiba
pikipiki tatu zilizokuwa zimehifadhiwa katika ofisi hiyo, viroba vitatu
vya mchele na boksi tano za tende.
Abbas Kilapo (aliye vaa kofia) akiwaonyesha Askari kanzu wa Kituo cha
Chang'ombe jinsi watuhao walivyofanikiwa kwa kuondoka na vitu hivyo
Muhusika wa ofisi hiyo ambaye alifahamika kwa jina la, Abbas Kilapo
akiwaonyesha Askari Kanzu na waandishi wa hapari (pichani hawapo) Namba za pikipiki na kadi za Pikipiki zilizo
ibiwa na watu wanaodaiwa ni wezi
Abbas Kilapo akizungumza na waandishi wa habari (pichani hawapo) mara baada ya kufika Ofisini hapo
Katibu
Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Miburani, Ally Kamtande
akimpepea mlinzi huyo Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
Sign up here with your email