Mtaalamu
wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, Hoyce Temu akiendesha mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu
Duniani (SDGs) kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma
mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali na
walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika jana chuoni
hapo.(Picha na Modewjiblog)
Mwanafunzi
wa Digrii ya kwanza ya Mifumo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM), Janeth Dutu akiuliza swali kwa mkufunzi wa mafunzo hayo (hayupo
pichani) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya
kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa
Dodoma ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini
na kumalizika jana chuoni hapo.
Sign up here with your email
