MKAZI WA KIGOMA AJINYONGA KWA KINACHOSADIKIWA KUWA WIVU WA MAPENZI - Rhevan Media

MKAZI WA KIGOMA AJINYONGA KWA KINACHOSADIKIWA KUWA WIVU WA MAPENZI



Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Norbert Gidion (30) mkaazi wa Masanga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  amekutwa  amefariki  dunia akiwa amejinyonga kwenye mti wa mwembe kwa kile kinachosadikika kuwa ni  wivu wa mapenzi
Kamanda wa polisi mkoani kigoma Afande Ferdinand Mtui, amethibitisha tukio hilo na kusemw kwamba upelelezi wa awali unaonesha kuwa  chanzo cha kifo cha Marehemu Norbert Gidion  ni  kutokuwepo na maelewano dhidi ya marehemu  na mke wake, Bi.Happyfania Caristus. 
"Natoa  wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa mazingira kama hayo husababisha kutokea vifo visivyotarajiwa kwa jamii:, alisema Kamanda Mtui.
Wakielezea tukio hilo wapangaji wenzie marehemu wamesema kuwa kwa kipindi kirefu marehemu alikuwa safari hadi umauti unamkuta na kwamba  hata alivyorudi safari alikuwa halali nyumbani kwa mke wake.
Mzazi wa marehemu Bw. Gidioni Hungu amesema  kuwa mazingira ya kifo hicho imekuwa sintofahamu kwani alikuwa hana maelewano mazuri na mkewe.



Previous
Next Post »