Refa
mmoja raia wa Sweden, alimpa kwa mpigo kadi mbili za njano mwanasoka
Adam Lindin Ljung-kvist, akiwa uwanjani, kwa kosa la kutoa hewa mbaya.
Mchezaji huyo alipokuwa katika
harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa kadi
nyekundu na kuondolewa uwanjani.
Refa
huyo ametaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi , kama tabia isiyo ya
mchezaji. Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo
kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa.
Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa
kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo
ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya
kuchafua hewa.
Amesema kuwa ameshangazwa sana na refa
kumtimua, huku akiongeza kuwa, kocha na wachezaji wenzake hawakuamini
walipomuona akirejea katika eneo la wachezaji wa ziada na kuwaambia kuwa
amepigwa kadi nyekundi kwa “kushuta.”
Adam, mwenye umri wa miaka 25 anaichezea timu ya Pershagen SK, inayo burura mkia katika ligi kuu nchini Sweden.
Sign up here with your email