Manji aliongeza kuwa, anataka kuendelea
kubaki Yanga ili kuiwekea mazingira ya kujitegemea na izidi kutisha
katika soka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam
katika kampeni zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaunda yalipo Makao Makuu
ya Yanga, Manji alisema aliikuta timu hiyo ikiwa haina maendeleo lakini
sasa inaogopwa.
“Tuliingia na ahadi ya kuzima utawala wa
Simba, wakati huo timu ilikuwa na migogoro, viongozi waliokuwepo
walikuwa wakilumbana. Ilikuwa Yanga mbovu, wengine wanajiuzulu.
“Lakini mimi na Sanga (makamu mwenyekiti
anayemaliza muda wake) kwa kuwa tulikuwa na mawazo sawa, tulipigana na
matunda yake ndiyo haya mnayoyaona,” alisema Manji.
Manji alisema endapo atachaguliwa tena,
atajitahidi kuweka mazingira ya Yanga kujitegemea ili iweze kufanya
mambo yake bila matatizo. Chini ya Manji, Yanga msimu huu imetwaa mataji
matatu ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la FA pia ipo
hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Naye Sanga anayetetea kiti chake,
akichuana na Titus Osoro alisema: “Mambo tuliyofanya ni ushahidi tosha,
nichagueni mimi na Manji tuendeleze haya mafanikio tuliyopata.”
Katika uchaguzi huo utakaofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, jumla ya wagombea 20 wanawania
nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ambapo wanahitajika nane tu.
Miongoni mwao ni, Lameck Nyambaya, Ayoub
Nyenzi, David Ruhago, Salum Mkemi, Samuel Lukumy, Tobias Lingalangala,
Beda Tindwa, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ na Hussein Nyika.
Sign up here with your email
