Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha
wanamaliza zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na
sekondari.
Mhe.
Suluhu ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa
wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi
kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha
amewaagiza viongozi hao kusoma alama za nyakati kwa kuangalia makosa ya
waliokuwepo kabla yao ili kuhakikisha hawarudii makosa yaleyale.
Mhe.Suluhu
pia amesema kuwa Serikali haitaki kusikia wananchi wanalia njaa na
hivyo wakuu wa wilaya wahakikishe chakula kinapatikana katika maeneo yao
kwani hilo ni jukumu lao.
Aliongeza
kuwa wakuu wa wilaya wana majukumu makubwa ya kuhakikisha wananchi
wanapata huduma zote za muhimu katika maeneo yao kwani wananchi wana
mategemeo makubwa juu yao.
Aidha
ameagiza wakuu wa Wilaya hao kufanya kazi karibu na Maafisa Tarafa ili
kujua kero za wananchi na kuzifanyia kazi kwa kasi ili wananchi
wafaidike na maendeleo yawafikie kwa haraka.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
George Simbachawene ivi karibuni aliwaagiza wakua wa wilaya na mikoa
kuhakikisha wanatimiza agizo la Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha
hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kwa uhaba wa madawati kufikia June
30,2016.
Sign up here with your email

