Leicester City, wamekubali kutoa ada ya uhamisho wa kiungo huyo anayeitumikia klabu ya Nice, inayotajwa kufikia kiasi cha Pauni milioni 13.
Mendy mwenye umri wa miaka 24, amekua katika rada za meneja wa Leicester City, Claudio Ranieri kwa majuma kadhaa sasa, na tayari imeanza kuonekana safari yake ya kucheza soka nchini England huenda ikakamilishwa ndani ya juma hili.
Kiungo huyo ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya AS Monaco, anatarajiwa kukabidhiwa mikoba ya kiungo mwenzake kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante ambaye anapigiwa hesabu na klabu za Arsenal na Chelsea zote za jijini London.
Sign up here with your email