KIUNGO mpya wa Wekundu wa Msimbazi Simba, Jamal Mnyate, ametangaza
vita ya kuwania namba dhidi ya wachezaji wanaocheza nafasi kama yake
katika kikosi cha timu hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC na Mwadui FC, amesema hataki
masihara linapokuja suala la kazi kwani lengo lake ni kuhakikisha
anapandisha thamani yake kama mchezaji.
Alisema anatambua timu yake hiyo mpya ina wachezaji wengi wazuri na wenye vipaji, lakini anaamini juhudi zake zitamshawishi kocha kuwa chaguo la kwanza.
“Nimejipanga kufanya vizuri ili kulipa fadhila ya wale walioniona kwamba nina uwezo, naamini juhudi zangu ndiyo silaha yangu itakayonifanya niaminiwe na kocha na nipate nafasi,” alisema.
Alisema licha ya kwamba kwa sasa ligi imesimama lakini kwa upande wake muda mwingi amekuwa akiutumia kujifua zaidi ili kuuweka mwili wake fiti.
“Mimi ni kama askari muda wote napaswa kuwa fiti, kwani mpira ni ajira yangu hivyo muda huu nautumia kwa kufanya mazoezi ya kujiweka imara ili ligi itakapoanza nifanye yangu,” alisema.
Alisema wachezaji wengi wanapokuwa mapumzikoni wamekuwa wakitumia muda huo kuponda raha lakini kwake hali ni tofauti kwani amekuwa akifanya mazoezi binafsi.

Sign up here with your email