Kipande
kipya cha mabaki ya ndege kilichopatikana nchini Tanzania kitafanyiwa
uchunguzi ili kubaini iwapo kinahusiana na mabaki ya ndege ya shirika la
ndege la Malaysia MH 370 iliyopotea na kutofahamika ilikoelekea hadi
hivi sasa.
Maelezo hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Malaysia ambalo
limemkariri waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo, Liow Tiong Lai, akisema
kuwa kipande hicho ni kikubwa na iwapo itathibitika kuwa ni cha ndege
hiyo basi nchi hiyo itatuma wachunguzi nchini ili kuchunguza iwapo ni
kweli kinahusiana na ndege ya MH 370 iliyopotea.
Aidha, Waziri Tiong Lai amesema mabaki ya ndege yaliyopatikana hivi
karibuni katika ufukwe wa bahari ya Hindi huko nchini Madagascar na
kufanyiwa uchunguzi hayakuwa na uhusiano wowote na ndege hiyo.
Sign up here with your email