JO COX ALIUAWA KATIKA SHAMBULIO MAALUM. - Rhevan Media

JO COX ALIUAWA KATIKA SHAMBULIO MAALUM.

Jo Cox aliuawa katika shambulio maalum

  • 18 Juni 2016
Image copyrightGETTY
Image captionJo Cox
Polisi wa Uingereza wanasema kuwa mbunge aliyeuawa, Jo Cox, aliuawa na watu waliomlenga yeye katika shambulio maalumu.
Wanasema kwamba wanaendelea kumhoji mshukiwa na kwamba wanadhani kuwa mshukiwa huenda alikuwa mmoja wa watu wenye mrengo wa kulia.
BBC inaelewa kwamba polisi walipata ishara za kundi la ubaguzi lenye asili ya Ujerumani la Nazi na maandishi ya kulitukuza kundi hilo nyumbani kwa Tom Mair.
Image captionJo Cox
Mapema Waziri Mkuu David Cameron na kiongozi wa upinzani wa chama cha Leba, Jeremy Corbin, walitoa heshima zao kwa Bi Cox, walipotembelea kijiji Kaskazini mwa England ambako Mbunge huyo alipigwa risasi na kudungwa kisu mnamo Alhamisi.
Previous
Next Post »