Je umeona sehemu ya chini ya kucha yako, ipo kama mwezi nusu, sehemu hiyo inaitwa lunula, kwa kweli ni eneo la muhimu sana na unapaswa kuhakikisha halipati uharibifu wa aina yeyote ile.
Hapa tunakwenda kuelezea mambo matano ya muhimu kujua kuhusu lunula:
1.Sehemu hii inonekana nyeupe,ni basal layer ya tano ya epidemis ambayo inaziba mishipa ya damu ambayo ipo chini.
2.Sehemu hii ya kucha inayoitwa lunula ni mzizi wa kucha na endapo ikiharibika au kuumia kwa namna yeyote ile, basi kucha yote itatoka.
3.Wataalamu wengi duniani kote wamegundua kwamba lunula inaeleza vizuri afya ya binadamu kwa ujumla. Kwa mfano, tiba za jadi za kichina wanaamini kwamba upungufu wa lunula inaonyesha dalili ya upungufu wa damu au utapiamlo, wakati pale au rangi ya blue ya lunula inaonyesha dalili ya ugonjwa wa kisukari. Kama lunula ina wekundu fulani basi huyo mtu atakuwa anasumbuliwa na magonjwa ya mishipa ya moyo.
4.Ukosefu wa lunula au lunula ni ndogo kuliko kawaida, inaonyesha indigestion ambayo inatokea kutokana na slow metabolism au kuzidi kwa sumu mwilini.
5.Kwa ujumla, Lunula inaeleza ugonjwa wa mtu kwa namna ya mabadiliko ya rangi au kwa kufifia zaidi au kutoonekana.
Baada ya mtu kupona maradhi yake basi lunula itaanza kuonekana tena.Udogo wa lunula mtu alionao, ni upungufu wa nguvu, afya mbaya na kinga ndogo mwilini, pia kuna uwezekano wa kujisikia uchovu. Kama lunula inaonekana kwenye kidole gumba tu, jua ya
kwamba nguvu katika mwili wako zimepungua na kuna ugonjwa unakunyemelea.
Sign up here with your email