MSANII wa
filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa anajuta kutofunga
ndoa na mkewe, Eva kwani anateseka sana kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan.
Akistorisha na gazeti hili, Dude alisema
kutokana na sheria za dini ya Kiislamu kwamba hairuhusiwi mwanaume
kupikiwa futari na mwanamke anayeishi naye tu bila kufunga ndoa, amekuwa
akiteseka kwenye suala la futari kwani mara nyingi anakula kwa mama
lishe.
“Najuta kutofunga ndoa na mke wangu
maana kila siku huwa nasema nitafunga leo mara kesho lakini miaka
imekuwa ikikatika tu sijui kwa nini, kama mwezi huu mtukufu nakula
futari kwa mama lishe huku nikiwa nalala chumba cha wageni mpaka mwezi
huu uishe,” alisema Dude.
Dude amekuwa akiahidi mara kwa mara
kwamba watafunga ndoa na mama watoto wake, Eva ambaye wanaishi pamoja
na wamejaliwa kupata watoto wawili kwamba watafunga ndoa lakini suala
hilo limegeuka kuwa kitendawili kwao.
Sign up here with your email
