CCM ZANZIBAR YAKATIKA VIPANDE VIPANDE. - Rhevan Media

CCM ZANZIBAR YAKATIKA VIPANDE VIPANDE.

Makundi mawili makubwa ya CCM Zanzibar yamejikuta yakiingia katika mgogoro mkubwa wa kimaslahi ambao unahusishwa moja kwa moja na Dokta Ali Muhammed Shein. Makundi hayo yanayojipanga kuwania uraisi Zanzibar 2020 yameanza kuvutana chini kwa chini kuhusu mambo mbali mbali yaliyotokea na yanaendelea kutokea Zanzibar katika masuala ya chama na uendeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ali Karume
Hayo yameibuka baada ya vigogo waliosababisha serikali kushindwa kukusanya mapato kutakiwa wajiuzulu baada ya kukosekana sehemu ya kuweka makontena zaidi ya 1,000 jambo lililosababishwa kwa kuuzwa kwa Hoteli ya Bwawani kwa maslahi yao binafsi bila kuwashauri watendaji wa Serikali wanaonufaika na Hoteli hiyo kama ilivyoripotiwa na Gazeti la Zanzibar Leo.
Zanzibar Leo1
Kuuzwa kwa hoteli ya Bwawani kwa Mfanya Biashara Yussuf Manji kunamhusisha moja kwa moja Dokta Ali Mohammed Shein na Balozi Seif Ali Idi.
Akichangia makadirio na mapato ya wizara ya miundo mbinu Zanzibar; Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Ndugu. Simai Mohamed Said (Mpakabasi) alisema serikali imeshindwa kukusanya mapato ya Sh. Bilioni 13 ya Makontena 3,300 kukwama kuteremshwa Bandari ya Malindi kufuatia sehemu ya kuhifadhi makotena hayo kuuzwa kwa Mfanya Biashara mmoja ili kujenga mradi wa Hoteli na maduka. Simai alisema ni jambo la kusikitisha viongozi wenye dhamana wameshindwa kutafuta eneo mbadala la kuhifadhi makotena kabla ya kuuzwa eneo ambalo walikuwa wakitumia Shirika la Bandari Zanzibar kuhifadhi makontena yasiyokuwa na Mizigo.
Balozi Seif Ali Idi, baada ya kutolewa hoja hiyo ndani ya Baaza la wawakilishi ameamua kujikosha kwa kutembelea Bandari na kutaka mrundikano wa makotena upatiwe ufumbuzi ili makotena yapelekwe viwanja vya mnazi mmoja.
Zanzibar Leo2Zanzibar leo3
Taarifa za mtandao wetu zinaeleza kwamba kundi la Balozi Ali Karume ndilo lililomtuma Ndugu. Simai Mohamed Said (Mpakabasi) kueleza suala hilo kwa lengo la kueleza ukweli wa kuuzwa kwa hoteli ya Bwawani kunakomhusisha Dokta Shein na Balozi Seif Ali Idi ambae atanufaika moja kwa moja na uuzwaji huo.
Mtandao wetu umethibitisha kwamba Ndugu Simai amekua akilalamika baada ya ahadi aliyopewa na Balozi Seif na Mkewe Bi Asha Balozi kwamba atapewa uwaziri baada ya uchaguzi wa March 2016 kuota mbawa.
Inaelezwa kuwa Simai alimpatia fedha zaidi ya milioni 20 Balozi Seif kwa ajili ya kampeni za kununua wapiga kura katika jimbo la Mahonda baada ya kura ya maoni kurejewa zaidi ya mara mbili bila ya mafanikio yoyote ya kumpatia ushindi kiongozi huyo wilaya ya Kaskazini B.
Vita ya Urais inakuja Baada ya Dokta Shein kushindwa kutekeleza ahadi yake kwa Balozi Ali Karume ambae alimtaka asaidie kuhujumu ushindi wa Maalim Seif ili wakifanikiwa amteue kuwa Makamo wa pili wa Rais nafasi ambayo Balozi Karume yeye na kundi lake wangeweza kuitumia ili kujenga mtandao wa kuukwaa Urais wa Zanzibar 2020, badala yake Dokta Shein amemrejesha Balozi Seif kinyume na ahadi yake kwa Balozi Ali Karume.
Kundi la Balozi Ali Karume ambalo linamhusisha Nadir Mustafa (Chaani), Raza, Simai (Mpakabasi), Said Soud, Suleiman Chotara (Mwakilishi wa Chake Chake) na Jazira ambae amekua akifanya kazi kinyemela na kundi hilo baada ya ahadi ya kupewa unaibu waziri wa wizara ya michezo kuota mbawa.
Kundi jengine ambalo linamtazama Balzozi kama mtu alieivuruga mihimili ya wanamapinduzi ni Haji Omar Kheri, Amina Salum Ali, Hamza Hassan Juma, Machano Khamis (Mwakilishi wa Mfenesini) ambalo limesikitishwa na baadhi ya viongozi wa muda mrefu kuangushwa baada ya kazi kubwa ya kuhujumu ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad wa Oktoba 25, 2015.
Hadi leo wanauliza imekuaje Ndugu. Pandu Ameir Kificho kunyimwa uspika baada ya kazi kubwa ya kumpatia Dokta Shein urais badala yake anapewa mtu ambae hajafanya kazi yoyote katika chama? Kundi hilo linajiuliza pia inakuwaje viongozi kama Dokta Mwinyi Haji Makame na Ramadhan Abdallah Shaaban nafasi zao zinaota mbawa na kupewa watu ambao hawakufanya kazi yoyote.
Wawikilishi kama Hamza Hassan Juma na Machano Khamis ambao walishinda viti vyao tokea uchaguzi wa oktoba 25, 2015 vipi wananyimwa nafasi badala yake viongozi wa vyama vitatu wanapewa nafasi kwa mapendekezo ya Balozi Seif bila ya kuwa na faida yoyote kwa CCM. Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu hadi leo anasikitika kwanini Mhe. Ali Juma Shamhuna amenyimwa nafasi ya uteuzi pamoja na mawaziri wenzake Mwinyi Haji Makame na Ramadhan Abdallah Shaaban wakati wamemsaidia kwa asilimia kubwa Dokta Shein kuiba haki ya Maalim Seif.
Previous
Next Post »