Vikosi vya Libya
vinavyoegemea serikali ya muungano mjini Tripoli vinasema kuwa
vimeichukua bandari ya mji wa sirte, kufuatia makabiliano makali baina
yao na wapiganaji wa Islamic state.
Msemaji wa kikosi hicho
jenerali Muhammad al-Ghusri anasema viongozi wakuu wa Islamic State
wametorokea jangwani, akiongeza kuwa wapiganaji wengi wa Islamic State
wamezingirwa mjini Sirte na kuwa makabiliano yanaendelea.Vikosi hivyo vinavyounga mkono serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli vilianza harakati za kuukomboa mji huo mwezi uliopita.
Sign up here with your email
