Patience Carter ni miongoni mwa watu walionusurika kifo kwenye tukio baya zaidi la mauaji ya bunduki nchini Marekani kwenye klabu ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Pulse Nightclub huko Orlando, Marekani. Yeye alipigwa risasi ya mguu.
Tukio hilo lililotokea June 12 lilisababisha vifo vya watu 50 na kuwaacha wengine zaidi ya 50 wakiwa majeruhi. “Niliweza kuona lundo la miili kwenye choo,” alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumanne hii.
“Kulikuwa na alama za mikono na damu. Niliangalia kwingine na niliona damu kila sehemu. Watu wengine walikuwa wamekufa na wengine wakilalamika kwa maumivu.”
Hapo ndipo msichana huyo mwenye miaka 20 alianza kusali. “Niliongea na Mungu. Nilisema ‘Mungu kama hivi ndivyo nitakufa, tafadhali chukua tu roho yangu kwenye mwili wangu.’ Nilitaka tu kufumba macho na kumwacha Mungu anichukue.”
Masaa manne baadaye, Carter na rafiki zake walikuwa bafuni na mtu huyo aliyekuwa na silaha. Katika kipindi hicho ndipo alipopiga 911 na kuonesha utii kwa ISIS. Baada ya kukata simu, muuaji huyo aitwaye Omar Mateen aliwauliza mateka swali.
“Kuna mtu yeyote mweusi hapa?” Carter anakumbuka mtu huyo kuuliza. Mtu mmoja alijibu kuwa alikuwa Ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika. “Sina tatizo na na watu weusi,” muuaji huyo aliwaeleza. “Hii ni kuhusu nchi yangu. Nyie watu mmeteseka vya kutosha.”
Carter, mkazi wa Philadelphia alikuwa Orlando kwa likizo. Aliifahamu Pulse nightclub kupitia Google Maps na kuamua kwenda na marafiki zake. Wakiwa chini bado, ghafla polisi walianza kuvunja ukuta. Mtu huyo alipata hasira zaid.
“Alipowasikia polisi nje, alisema ‘Hey, you!’ kwa mtu aliyekuwa chini na kuwapiga risasi. Alimpiga mwingine, kisha mwingine aliyekuwa kulia kwangu. Miili yao ilinikinga na risasi.”
Mmoja wa marafiki wa Carter, Tiara Parker, alijeruhiwa lakini ni mzima. Rafiki yake mwingine Akyra Murray, aliuawa.

Sign up here with your email