Jeshi la polisi jijini Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya uporaji na mauaji ya wafanyabiashara jijini Mwanza katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wapolisi jijini Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika nyumba moja eneo la Bukarika Jijini humo.
Watu hao wamekamatwa na bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 144 ambapo jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi kuweza kuwakamata watu wote ambao wanajihusuisha na mtandao wa ujambnazi.
Aidha kuanzia mwezi Februari hadi sasa wafanyabiashara 18 wanaofanya kazi ya mitandao ya kutoa na kubadilisha pesa wameuawa jambo ambalo limesababisha hofu kubwa kwa wananchi.
Sign up here with your email