Waandishi wa habari binafsi raia wa Uhispania waliotekwa nyara nchini Syria miezi kumi iliyopita wameachiliwa huru.
Mara ya mwisho walionekana Aleppo, ambako walikuwa wakiripoti kuhusiana na matukio jijini humo Julai, mwaka uliopita.
Gazeti la Uhispania la El Pais lilisema kuwa wanaume hao watatu- Antonio Pampliega, José Manuel López and Ángel Sastre - wakati huu wako Uturuki ambako wanasubiri kurudi nyumbani.
Serikali ya Uhispania imesema kuwa Uturuki, Qatar na mataifa mengine ambayo imetaja kama marafiki yalichangia pakubwa katika kuhakikisha kuwa waandishi hao wameachiliwa.
Hakuna habari zaidi zilizotolewa.
Chama cha waandishi wa habari cha Uhispania kimesema kuwa habari hizo ni za kufurahisha na kutia moyo.
Rais wa chama hicho, Elsa Gonzalez, alisema kuwa kazi ya waandishi wa habari kama hawa imeimarisha sifa ya kazi ya waandishi.
Sign up here with your email