WAKAZI WA MJI MZIMA WAKIMBIA MOTO CANADA - Rhevan Media

WAKAZI WA MJI MZIMA WAKIMBIA MOTO CANADA

Moto mkubwa wa nyika umelazimisha kuhama watu 60,000 kutoka mji wa Fort McMurray ambao ni idadi yote ya wakazi wa mji huo wa nchini Canada.
Ndimi za moto zimeteketeza nyumba kadhaa, na kushusha majivu kwenye mitaa katika mji huo uliopo kwenye mkoa wa Alberta.
Wakazi wanaokimbia mji huo wamesababisha foleni kubwa katika barabara kuu inayotoka kwenye mji huo uliopo kilomita 380 kaskazini mwa Edmonton.
Previous
Next Post »