Mjumbe wa nyumba kumi wa Mtaa wa Majengo Sokola, Juma Jacob alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Diwani wa Kata ya Nyangh’wale mkoani Geita aliyemtaja kwa jina moja la Kamuli ambako mwanamke huyo amepanga.
Hata hivyo, mama huyo alikosa kiasi hicho cha fedha kabla ya kujitokeza kwa jirani aliyemsaidia huku mwenyewe akilaumu kitendo alichofanyiwa kwani hakikuwa cha kibinadamu hasa kwa kuwa ana majonzi makubwa kwa msiba wa mwanaye wa pekee uliomkuta.
Mtoto Vero alikutwa akiwa amefariki katika dimbwi la maji majira ya saa moja na nusu usiku wa Jumanne iliyopita, baada ya mama yake pamoja na majirani kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambalo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa Majengo na kwamba hakuna mtu yeyote anayeshukiwa kusababisha kifo hicho. Aliwataka wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao wadogo hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo Sokola, Mary Sumuni aliwaagiza viongozi wa jumuiya za mtaa huo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kufukia madimbwi yote yaliyochimbwa kwa lengo la kutupia takataka, na kwamba atakayekiuka atafikishwa mahakamani.
Aliwataka wananchi wa mtaa wake kuacha tabia ya kuchimba makaro ya vyoo na kuyaacha wazi, kwani pasipo kuziba vifuniko vyake, ni rahisi kwa watoto kutumbukia wakati wakicheza.
Sign up here with your email