Mwili wa mke wa Rais wa Kenya mstaafu Mhe. Mwai kibaki , Mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa ajili ya mazishi hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mhe. Mwai Kibaki katika mazishi ya mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi, Kenya. Anayeshuhudia katikati ni Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta.
Naibu Rais wa Kenya Mhe.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mhe.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi. Kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta, Mama Margaret Kenyatta.
Rais Mstaafu wa Kenya, Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mhe. Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki. Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Mama Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Marehemu Mama Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.
Dkt. Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy Kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.
Sign up here with your email