Na Bashir Yakub.
1.MIRATHI NI NINI.
Mirathi ni mali ya marehemu aliyoiacha kwa ajili ya kurithisha warithi wake halali. Hakuna mirathi kabla ya kifo cha mtu. Ni lazima mtu afe ndipo ipatikane mirathi. Na mirathi kwa ujumla wake huhusisha mali alizoacha marehemu.
2. NINI LENGO LA UTARATIBU WA MIRATHI.
Lengo kuu la kuwepo utaratibu maalum wa mirathi ni kukusanya, kuangalia, kusimamia, na kugawa mali alizoacha marehemu. Kulipa madeni aliyoacha marehemu na kujua madeni hayo yalipo nalo ni lengo la kuanzishwa utaratibu huu wa mirathi.
Lakini jingine katika hili ni kusimamia shughuli za mazishi ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo ya marehemu kuhusu namna na wapi azikwe. Hizi zote ni shughuli zilizopelekea kuanzishwa utaratibu wa mirathi.
Kama utaratibu huu usingewekwa na sheria basi ingekuwa rahisi mali za marehemu kupotea hovyo,kuharibiwa, kutumiwa vibaya na kuhujumiwa.
Lakini ingekuwa rahisi kwa wale wote wanaomdai marehemu kupoteza haki zao za madai baada ya kufa. Lakini kwa utaratibu maalum wa mirathi hawa nao hawawezi kupoteza haki zao.
3. NI SHERIA ZIPI HUTUMIKA KATIKA MIRATHI.
Hapa Tanzania zipo sheria tofauti tatu zinazotumika katika mirathi. Ipo sheria ya serikali, zipo sheria za kimila na zipo sheria za dini ya kiislamu. Makala ya leo hayataingia ndani zaidi kueleza sheria hizi. Kwa leo itoshe kujua tu kuwa sheria zinazotumika kwa hapa kwetu ni hizo tatu.
Sign up here with your email