COMERON : NIGERIA NI MAFISADI WAKUU DUNIANI. - Rhevan Media

COMERON : NIGERIA NI MAFISADI WAKUU DUNIANI.

Image copyrightAFP
Image captionDavid Cameron akimweleza malkia Elizabeth ' Nigeria na Afghanistan ni mafisadi wakuu duniani''
Mzozo wa kidiplomasia unatokota baada ya Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kunaswa kwenye Kamera akimwambia Malkia Elizabeth wa Pili kuwa viongozi wa mataifa mawili yenye ufisadi mkubwa kote duniani Nigeria na Afghanistan watakuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika kongamano la kupambana dhidi ya zimwi la ufisadi litakalofunguliwa siku ya Alhamisi mjini London.
Matamshi hayo ya Cameron yalitolewa katika kasri la Buckingham bw Cameron alipokuwa amekwenda kumtembelea malkia Elizabeth katika sherehe ya kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.
Image copyrightAFP
Image captionAskofu mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anasikika akimkumbusha Waziri mkuu bw Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.
Aidha Cameron alieelezea malkia Elizabeth jinsi mataifa hayo yalivyosakamwa na viongozi mafisadi.
Kiongozi wa kanisa la kianglikana Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anasikika akimkumbusha Waziri mkuu bw Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.

Image copyright
Image captionAidha Cameron alieelezea malkia Elizabeth jinsi mataifa hayo yalivyosakamwa na viongozi mafisadi.
Afghanistan iliorodheshwa katika nafasi ya 167, nafasi moja pekee mbele ya Somalia na North Korea, katika orodha ya 2015 ya shirika la kupambana na ufisadi duniani Transparency International .
Nigeria iliorodheshwa katika nafasi ya 136.
Previous
Next Post »