Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda aliwaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe.
Leo May 09 2016 katika uchunguzi wa awamu ya tatu wamekuja na ripoti ya watumishi hewa 39 walioisababishia Serikali hasara ya BILIONI 3.6.
Paul Makonda amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Manispaa ya Ilala, Gerac Phus kwa kutowagundua watumishi hewa 11 ambao walikuwa hawajulikani wapo idara gani.
Sign up here with your email