YANGA YATUA MWANZA KUMALIZANA NA TOTO JUMAMOSI. - Rhevan Media

YANGA YATUA MWANZA KUMALIZANA NA TOTO JUMAMOSI.

Klabu ya Yanga imewasili jijini Mwanza leo Asubuhi kwa ndege kwa ajili ya mechi zake mbili mfululizo za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Kanda ya Ziwa.
Baada ya jana kuendeleza desturi ya ushindi katika ligi hiyo kwa kuifunga Mgambo JKT 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga inatarajiwa kucheza na Toto Africans Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Na baada ya hapo, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, Mei 3 watakuwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kumenyana na wenyeji Stand United katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.
Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wake wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola Mei 8, Uwanja wa Taifa.
 
Yanga inahitaji ushindi angalau wa mechi tatu zilizosalia ili ijihakikishie ubingwa wa pili mfululizo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Previous
Next Post »