(WHO) YEMEN INAKUBWA NA MAAFA YA KIBINADAMU. - Rhevan Media

(WHO) YEMEN INAKUBWA NA MAAFA YA KIBINADAMU.


Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Yemen amesema asilimia 80 ya watu wa nchi hiyo wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Dr. Ahmed Shadoul, ametangaza kuwa watu milioni 19, ambao ni sawa na asilimia 80 ya wananchi wote wa Yemen wanahitaji misaada ya kimataifa; na Wayemeni milioni 14 hawapati huduma za msingi za afya na tiba.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa WHO nchini Yemen, asilimia 28 ya taasisi za afya na tiba nchini Yemen hazifanyi kazi na asilimia 14 zinafanya kazi kwa kiwango cha chini ya asilimia 50; na hiyo ni hali ya kutisha.

Wakati huohuo tovuti ya habari ya Akhbarus Saa'ah imeripoti kuwa maelfu ya wakimbizi wa Yemen waliokimbilia nchini Djibouti kuomba hifadhi kutokana na uvamizi wa kijeshi ulioanzishwa na Saudi Arabia mwaka mmoja uliopita dhidi ya nchi yao, wako katika hali mbaya.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa maelfu ya raia hao wa Yemen wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku wakiishi katika mazingira hatarishi ya anuai za magonjwa, ukosefu wa chakula na maji na hali mbaya ya kiafya.

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa vita vilivyoanzishwa na utawala wa Aal Saud dhidi ya Yemen, zaidi ya raia laki moja na elfu 73 wameihama nchi hiyo, ambapo elfu 33 kati yao wamekimbilia nchini Djibouti.

Kwa mujibu wa tovuti ya Akhbarus Saa'ah, kila wiki, raia kati ya 500 hadi 800 wa Yemen wanakimbilia nchini Djibouti kujinusuru na maafa ya mashambulio ya anga ya ndege vamizi za Saudia na washirika wake. Hata hivyo raia hao wanaishi katika mazingira mabaya yasiyo na suhula wala huduma zozote za msingi zikiwemo za chakula, maji na dawa wala hifadhi ya 
Previous
Next Post »