WAYEMENI WA GUANTANAMO WAPELKWA SAUDIA. - Rhevan Media

WAYEMENI WA GUANTANAMO WAPELKWA SAUDIA.


Image copyrightUnited States Department of Defense
Image captionWayemeni wa Guantanamo wapelekwa Saudia

Makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon, imesema wafungwa 9 wa Yemeni waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay sasa wamehamishiwa nchini Saudi Arabia.
Maafisa wa Marekani wanasema wameamua kuwapeleka wafungwa hao Saudia kwa sababu Yemen ingali inakabiliwa na mzozo wa kisiasa, na pia baadhi ya wanafamilia wao wako Saudia.
Mmoja wa wafungwa hao ni yule aliyekuwa akitumia njia ya kususia chakula mda mrefu akipinga kuzuiliwa kwake.

Image copyright
Image captionRais Obama anataka kulifunga gereza hilo la Marekani lililoko Guantanamo Cuba.

Kundi hili likishaondoshwa , Wafungwa 80 ndio idadi ya watakaosalia huko Guantanamo ambako wamekuwa wakizuiliwa pasi na kufunguliwa mashtaka kwa mda wa zaidi ya miaka 10 iliyopita. .
Rais Obama anataka kulifunga gereza hilo la Marekani lililoko Guantanamo Cuba.
Previous
Next Post »