Msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo
jana asubuhi ulipotea njia kutokana na watumishi wa Manispaa ya Dodoma
kutojua eneo ambalo waziri huyo alikuwa analitembelea.
Waziri Jafo
alikuwa amepanga kufanya ziara kwenye Shule ya Msingi ya Nzuguni B kwa
lengo la kuangalia mapungufu, hasa tatizo la uhaba wa madawati, lakini
hakufika kama alivyotarajia kutokana na watumishi hao kutojua eneo
ambalo shule hiyo iko.
Shule hiyo haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha ya kuwa kilomita 6 kutoka katikati ya mji.
Naibu
Waziri alikasirishwa na kitendo hicho akawataka watumishi wa idara ya
Elimu wajipime kama wanastahili kuendelea kufanya kazi.
Sign up here with your email