WANAKIJIJI WAVUNJA MKUTANO BAADA YA KUGUNDUA VIONGOZI MAJIPU. - Rhevan Media

WANAKIJIJI WAVUNJA MKUTANO BAADA YA KUGUNDUA VIONGOZI MAJIPU.

Mkutano Mkuu wa kijiji cha Mgwasi kata ya Makanya wilaya ya Same wa kujadili kero za wananchi umevurugila baada ya mwenyekiti wa kijiji kukataa kujadili ajenda ya kuuzwa kwa eneo la hekta nane linalo chimbwa  madini ya Road Light ambalo viongozi wa kijiji wanadaiwa kuliuza kwa mwekezaji  kwa kiasi cha shilingi laki sita na wananchi wametoa wiki mbili za mwekezaji huo kuondoka kwenye eneo ilo la sivyo watafanya maamuzi magumu.
Katika mkutano huo uliohudhuliwa na idadi kubwa ya wakazi wa kijiji cha Mgwasi uligubikwa na sintofahamu baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho Abraham Arevo  kuwakilisha hoja moja tu ya Madawati badala ya kujadili kero ya kuuzwa kwa ardhi  kisha wananchi wakaikataa hoja hiyo kuwa siyo kero yao  na  wakataka kupata maelezo ya  ardhi hiyo ya  kijiji inayodaiwa kuuzwa kinyemera. 
Wakizungumza baada ya kuvunjika kwa mkutano huo wananchi walioonekana kuwa na jazba wamesema awakubaliani na hatua ya viongozi wa kijiji kuuza ardhi ya wananchi tena eneo lenye madini kwa mkataba wa kujengewa Choo cha shule kwa ghalama la shilingi laki sita.
Afisa Mtendaji wa kata ya Makanya Ramadhani Bakari amesema alivyo hamia kwenye Kata hiyo alikuta mkataba umeshasainiwa na alimwita mwekezaji na  mwekezaji alionesha nyaraka halali ikiwemo leseni ya uchimbaji  hata hivyo ITV inafanya juhudi za kumtafuta mwekezaji wa kampuni ya Hamex General Trading  Company ili kupata ukweli wa jambo ilo baada ya kutokuwepo kwenye mkutano huo  wa kijiji.
Previous
Next Post »