WANAFUNZI 700 WANAKAA CHINI SHULE MOJA -RORYA. - Rhevan Media

WANAFUNZI 700 WANAKAA CHINI SHULE MOJA -RORYA.


Wanafunzi 700 wa shule ya msingi Nyamugere iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara wanakaa chini kutokana na upungufu wa madawati jambo linalowafanya kutoshiriki vyema masomo na kufanya vibaya kitaaluma huku wengi wakiwa watoro.
Wakizungumza shuleni hapo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo wanafunzi hao wamesema wanakaa chini kutokana na ukosefu wa madawati shuleni hapo jambo linalowakwamisha katika maendeleo ya kitaaluma.
Kwa upande wake mmoja wa walimu shuleni hapo mwalimu Marco Lucas amesema shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa miondombinu ikiwemo ukosefu wa nyumba ya walimu ambapo wao wanakaa mbali sana na shule jambo linalowapunguzia pia morali ya kazi.
Kutokana na upungufu huo wazazi wa wanafunzi hao wamesema hawatachangia maendeleo ya shule hiyo kwa kuwa michango waliyochanga awali ililiwa bila madawati kutengenezwa.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo ameagiza wakurugenzi wa elimu kuhakikisha wanafanya ukaguzi katika shule na kubaini changamoto zilizopo ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati huku Mkuu wa Wilaya ya Rorya Felix Lyaniva akisisitiza upatikanaji wa madawati kabla ya mwezi Juni kama alivyoagiza Rais Dkt. John Magufuli.
Previous
Next Post »